SERA YA FARAGHA
Tafadhali soma sera hii ya faragha kwa umakini kwasababu inaelezea sisi ni nani na tunapakuaje na kuzitunzaje taarifa zako, na tunazitumiaje. Pia inazungumzia haki ulizonazo kuhusiana na suala hili la taarifa (data). Tafadhali angalia vichwa vya Habari hapo chini uweze kusoma kwa undani kuhusu kila moja ya maeneo tuliyoyataja.
Tafadhali tumia faharasa iliyo ndani ya nyaraka hii kuelewa maana ya baadhi ya maneno tuliyotumia.
Sera hii ya faragha inatolewa kwa niaba ya World Mobile Chain Ltd. Hivyo tunaposema “sisi,” au “ya kwetu” katika sera hii, tunarejelea kampuni husika katika umoja wa makampuni yetu inayohusika na jukumu la kuchakata data. World Mobile Chain Ltd ndio wanaowajibika na tovuti hii.
Wasiliana nasi
Tumeteua afisa wa kulinda data (DPO) aliye na jukumu la kujibu maswali yanayohusiana na hii sera. Kama una maswali yoyote kuhusu sera hii, Pamoja na maombi yoyote ya kusimamia haki zako, tafadhali wasiliana na afisa huyu kutumia mawasiliano hapo chini.
Afisa Ulinzi wa Data: | Enrique Opi |
Office: | 6th floor, Block C, Plot no:198 Michenzani Mall, Mjini Magharibi, P.O Box 3850, Unguja, Zanzibar. |
Content
1. Taarifa muhimu na utambulisho wetu
Purpose of this privacy policy
Madhumuni ya sera hii ya faragha
Sera hii inalenga kukutaarifu namna World Mobile Chain Ltd inakusanya na kuchakata taarifa zako binafsi kupitia tovuti yetu. Hii unajumlisha taarifa zozote utakazotoa kupitia tovuti yetu pale unapolipia huduma au bidhaa.
Ni muhimu sana usome sera hii pamoja na sera nyingine yoyote ya masuala ya faragha tutakayokupatia katika nyakati maalumu tunapokusanya au kuchakata taarifa zako binafsi ili uwe na taarifa kamili ya jinsi tnavyotumia taarifa zako na kwanini tunazitumia. Sera hii inachangia sera nyingine na lengo lake sio kupangua sera hizo.
Msimamizi.
World Mobile Chain Ltd ni kampuni ya BVI limited inoshughulika na mawasiliano ya kimataifa. World Mobile Chain Ltd itashughulika na kuwajibika na data zako binafsi.
Wajibu wako kututaarifu kuhusiana na mabadiliko
Ni muhimu sana kuhakikisha taarifa zako tulizonazo ni sahihi na za wakati wasasa. Tafadhali tujulishe kama kutakuwa na mabadiliko yoyote katika taarifa zako kipindi chote cha mahusiano yako na sisi.
Viungo vya Wahusika wa Watatu
Tovuti hii inaweza kuwa na viungo vya wahusika wa tatu, programu-jalizi na programu. Kugusa viungo hivyo kunaweza kuruhusu wahusika wa tatu kukusanya au kusambaza taarifa zako. Hatumudu tovuti za wahusika wa tatu na hatuwajibiki na sera zao za faragha. Unapotoka Kwenye tovuti yetu tunakushauri usome kila sera ya faragha Kwenye tovuti zote utakazotembelea.
2. Data zako tunazozikusanya
Tunaweza kukusanya taarifa zako binafsi tunavyoendelea na shughuli zetu, kupitia matumizi yako ya tovuti yetu, pale unapowasiliana nasi na unapoomba taarifa kutoka kwetu, pale unapojihusisha na huduma zetu au kupitia mahusiano yako na mfanyakazi au wafanyakazi wetu.
Taarifa zako binafsi tunazochakata hujumuisha:
- za utambulisho hujumuisha jina la kwanza, jina la ukoo ulikozaliwa, jina la mwisho/jina la ukoo, jina la matumizi, hali ya mahusiano yako, tarehe ya kuzaliwa na jinsia yako.
- Data za Mawasiliano hujumuisha anuani ya malipo, anuani ya makazi, barua pepe na namba za simu.
- Data za Kifedha hujumuisha taarifa za akaunti yako ya benki na taarifa za kadi ya malipo.
- Data za malipo hujumuisha taarifa za malipo kuja kwako na kutoka kwako na taarifa nyingine kuhusu bidhaa au huduma ulizonunua kutoka kwetu.
- Data za Kiufundi hujumuisha anuani ya protokali za mtandao (IP), taarifa zako za kuingia, aina ya programu-jalizi ya kivinjari, jimbo la muda wako, eneo ulilopo, aina ya kivinjari, mfumo wa kuongoza na teknolojia nyigine Kwenye kifaa unachotumia kuingia kwenye tovuti.
- Data za Wasifu hujumuisha jina unalotumia na neno la siri, manunuzi na oda ulizozifanya, vitu unavyopenda, mrejesho na majibu yako ya dodoso.
- Data za Matumizi hujumuisha taarifa za jinsi unavyotumia tovuti yetu, bidhaa zetu na huduma zetu.
- Data za Masoko na Mawasiliano hujumuisha mapendeleo yako ya jinsi unataka kupokea matangazo kutoka kwetu na vikundi vyetu vya tatu.
Taarifa hizi binafsi zinahitajika ili kutuwezesha kutoa huduma zetu kwako. Usipotoa taarifa zako binafsi, itatuchelewesha au kutuzuia kukupa huduma.
Pia tunakusanya, kutumia na kusambaza Data za Ujumla kama vile takwimu kwa madhumuni mbalimbali. Data hizi za ujumla zinaweza kutoka Kwenye taarifa zako binafsi. Kwa mfano, tunaweza kujumuisha taarifa zako za matumizi kupata asilimia ya watumiaji wanaopata huduma Fulani katika tovuti yetu. Walakini, tukijumuisha taarifa zako na data za ujumla ili kuweza kukutambua, tunaziangalia data hizo za jumla kama taarifa binafsi zinatakazotumika sambamba na sera hii ya faragha.
Hatukusanyi Vipengere Maalumu vya Data Binafsi zinazokuhusu (hii unajumuisha taarifa kuhusu rangi yako, kabila lako, dini yako au Imani yako ya kifalsafa, taarifa zako za kujamiiana, jinsia yako, itikadi yako ya kisiasa, uanachama kwenye vyama vya wafanyakazi, taarifa kuhusu afya yako, pamoja na taarifa zako za kibayometriki) Pia hatukusanyi taarifa zako zinazohusu vifungo vya kihalifu.
Ukishindwa kutupatia data binafsi
Tunapohitaji kukusanya data kisheria au chini ya masharti ya mkataba tulionao kati yetu na wewe, na unashindwa kutupatia data hizo tunapokuomba, hatutaweza kutimiza wajibu wa mkataba tulionao kati yetu na wewe (mfano ni kukupatia bidhaa au huduma) Katika suala kama hili inatubidi kusitisha huduma an bidhaa tunayokupatia, lakini tutakujulisha ikiwa hii ndio hatua tutakayochukua
3. Jinsi tunavyotumia data zako binafsi
Tutatumia data zako binafsi pale tu sheria inapoturuhusu. Kimsingi, tutamia data zako katika mazingira yafuatayo:
- Where we need to perform the contract we are about to enter into or have entered into with you.
- Where it is necessary for our legitimate interests (or those of a third party) and your interests and fundamental rights do not override those interests.
- Where we need to comply with a legal obligation.
Kwa kawaida, hatutegemei ridhaa kama msingi wa kisheria kuchakata data zako binafsi japokuwa tutapata ridhaa yako kabla ya kutuma data zako kwa wahusika wa tatu kinachoshughulika na masoko na mawasiliano kupitia barua pepe na ujumbe wa simu. Una haki ya kusitisha ridhaa yako kutoka masoko kwa kuwasiliana na sisi.
Madhumuni yanayotuongoza katika kutumia data zako binafsi
Tumeweka hapo chini katika mfumo wa jedwali, maelezo ya namna mbalimbali ya jinsi tutakavyotumia data zako na misingi ipi ya sheria tunaisimamia katika kutekeleza hilo. Na pia tumeidhinisha shughuli zetu za kihalali ambazo tungependelea kujihusisha nazo.
Tambua kuwa tunaweza kuchakata data zako binafsi kwa kuzingatia zaidi ya msingi mmoja wa sheria kutokana na madhumuni mbalimbali yanayotuongoza katika kutumia data zako.
Kama tutapokea data zako moja moja kutoka kwako au kutoka kwa kikundi cha tatu, tutatumia data zako pale tu tunapokuwa na sababu ya msingi ya kufanya hivyo, mfano.: kutimiza wajibu wetu kimkataba kwako wewe au kuchukua hatua kwa muongozo wako wewe mwenywe kabla kuingia Kwenye mkataba; Kwa shughuli zetu halali au za wahusika wa tatu zinazohitaji data zako binafsi; au pale ulipotoa ridhaa. Tunaweza kutumia data zako binafsi, kwasababu zifuatazo tu. (Madhumuni Yaliyoruhusiwa)
- Pale ambapo tunahitajika kutimiza majukumu yetu katika mkataba tunaotaka kuingia au mkataba tulioingia tayari kati yetu na wewe.
- Pale ambapo kuna umuhimu katika shughuli zetu (au za wahusika wa tatu) na mapenzi yako na haki za msingi hazipingi shughuli hizo.
- Pale ambapo inabidi kusimamia majukumu ya sheria
- Kwa madhumuni yoyote yanayohusiana na yoyote kati ya tuliyoyataja hapo juu au kwa madhumuni yoyote yale yaliyopelekea data zako kutufikia.
Kujitoa
Tunaweza kutumia utambulisho wako, mawasiliano yako, matumizi ya kiufundi pamoja na data za wasifu kutengeneza mtazamo utakaotujulisha utapenda au kuhitaji nini. Hivi ndivyo namna tunaamua bidhaa, huduma na ofa gani zitakuwa zinakuhusu zaidi (Hii tunaita masoko) Utapokea taarifa za matangazo kutoka kwetu ikiwa umeomba taarifa kutoka kwetu au umenunua huduma au bidhaa kutoka kwetu na hukusema hutaki kupokea matangazo hayo.
Tuna madhumuni halali ya kuchakata data zako binafsi kwa madhumuni ya matangazo. Hii humaanisha kuwa hatuhitaji ridhaa yako kukutumia jumbe za matangazo. Walakini, pale ridhaa inapohitajika, tutaomba ridhaa hiyo kivyake na kwa uwazi kabisa. Pia tutakubaliana na maagizo yako kuwa tuache kukutumia jumbe za matangazo.
Tutaheshimu data zako kwa viwango vya juu kabisa na hatutauza wala kuzitoa kwa mashirika mengine nje ya World Mobile Chain Ltd Ltd kwa madhumuni ya kutangaza isipokuwa pale tu ulipotupa ridhaa yako.
Una haki ya kujitoa kupokea jumbe za matangazo muda wowote kwa kututumia barua pepe.
Kujitoa
Unaweza kutuuliza sisi au wahusika wa tatu kuacha kukutumia jumbe hizo za matangazo muda wowote kwa kuwasiliana na sisi.
Unapojitoa kupokea jumbe hizi za matangazo, hili halitaingiliana na data zako binafsi zinazotokana na manunuzi yako ya huduma au bidhaa zetu, kujiandikisha katika udhamini, Pamoja na manunuzi mengine. Vidakuzi
Unaweza kuweka kivinjari chako kikatae baadhi ya vidakuzi au vidakuzi vyote, au kukujulisha pale tovuti zinapoweka vidakuzi. Unapositisha au kukataa vidakuzi, tambua kuwa baadi ya sehemu kwenye tovuti hii zinaacha kuingilika au kutofanya kazi vizuri. Mabadiliko ya Madhumuni
Tutatumia data zako binafsi kwa madhumuni yaliyotupelekea kuzikusanya, isipokuwa tu pale tutakapoona haja ya kutumia kwa madhumuni ya tofauti, na madhumuni hayo yawe yamefanana na madhumuni mama. Ukitaka kupata maelezo ya namna gani kuchakata kwa madhumuni mapya ni sambasamba na madhumuni mama, tafadhali wasiliana nasi.
Kama tunahitaji kutumia data zako binafsi kwa madhumuni yasiohusiana, tutakujulisha na tutatoa maelezo ya misingi ya kisheria inayoturuhusu kufanya hivyo.
Tafadhali tambua kuwa tunaweza kuchakata data zako binafasi bila utambuzi wako wala ridhaa yako, tukienda sambasamba na sheria tajwa hapo juu, ambapo jambo hili huzingatiwa na kuruhusiwa na sheria.
4. Kuidhinisha data zako binafsi
Tunaweza kutoa taafira zako binafsi kwa wahusika wa tatu tunaowaamini kama sehemu ya makubaliano ya kisheria, ikiwemo:
- Washauri wetu wa kitaalamu
- Watoa huduma tunaowapa kazi mbalimbali
- Watu wetu wa bima na mawakala
- Benki zetu
- Mahakama, vyombo vya dola, mamlaka za kisheria katika kutimiza wajibu wetu kisheria. Tutatumia mbinu za kudhirisha kukujulisha kabla hatujafanya hivi, isipokuwa tu pale tutakapozuiliwa kufanya hivyo kisheria.
- Wahusika wa tatu wakihusika katika kuandaa na kusimamia shughuli au semina.
- Kwa wahusika wa tatu ambao tunaweza kuamua kuwauzia, kujiunga nao na kuhamisha sehemu ya biashara au mali zetu. Pia tunaweza kutaka kununua na kujiunga na biashara nyingine. Kama kuna mambo yatabadilika katika biashara yetu, basi wamiliki wapya watatumia data zako kama ilivyowekwa wazi katika sera ya faragha.
Pale ambapo tutatoa au kuhamisha data zako binafsi, tutafanya hivyo kulingana na sheria za ulinzi wa data zinazohusika na tutachukua hatua salama kuhakikisha zinalindwa.
5. Uhamisho wa Kimataifa
Wengi wa wahusika wa tatu wa nje wapo nchini Tanzania hivyo uchakataji wao wa data utahisha kuhamisha data zako kwenda nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kila tunapotoa data zako binafsi nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunahakikisha kuna ulinzi ulele tulioahidi kwa kuzingatia angalua hatua mojawapo kati ya hizi zifuatazo imechukuliwa
- Tutatoa data zako kwenda Kwenye nchi zinazotoa ulinzi wa kutosha kwa data zako binafsi.
- Pale tunapotumia baadhi ya watoa huduma, tunaweza kutumia mikataba iliyoidhinishwa kwa matumizi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa ulizi ulele kwa data binafsi kama nchini Tanzania.
Tafadhali wasiliana nasi kama unahitaji taarifa za ziada kuhusu mbinu maalumu tunazotumia pale tunapohamisha data zako kwenda nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
6. Ulinzi wa Data
Tumeweka ulinzi kama tahadhari ya kuepusha mambo kadha wa kadha, ikiwemo; data zako kupotea katika ajali, data kutumika au kupatikana katika namna isiyoidhinishwa, kuchezewa na kuanikwa. Na zaidi ya hapo tunahakikisha nje ya wanohitaji data zako binafsi kama vile wafanyakazi, mawakala, wakandarasi, na wahusika wa nje wa tatu wenye mahitaji ya kujua. Watachakata data zako kwa kuzingatia maelekezo yetu na ni lazima wazingatie usiri.
Tumeweka taratibu za kushughulika na uhalifu wa namna yoyote unaovunja makubaliano ya data tuliyoweka na tutakujulisha juu ya tukio hilo pale sheria inapotuongoza kufanya hivyo.
7. Kuhifadhi Data
Utatumia data zangu binafsi kwa muda gani?
Tutahifadhi data zako binafsi kwa kipindi ambacho tutakuwa na madhumuni na data hizo, ikiwemo madhumuni ya kutimiza wajibu wa kisheria, kodi, au mahesabu. Tunaweza kubaki na data zako binafsi kwa muda mrefu zaidi pale tunapopokea lawama au pale tunapodhania kuna uwezekano wa kesi inayohusisha mahusiano yetu.
Kujua muda sahihi wa kutunza data zako binafsi, tunazingatia idadi, asili na unyeti wa data hizo, hatari inayoweza kutokea kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya data hizo, pia tunazingatia madhumuni ya sisi kuchakata data hizo na kama tunaweza kutimiza madhumuni hayo kwa mbinu nyingine, na majukumu ya kisheria, kodi, mahesabu na mengineyo.
Kutokana na sheria inatubidi tutunze taarifa za msingi kuhusu wateja wetu (ikiwemo mawasiliano, utambulisho, data za kifedha na mahesabu) kwa miaka sita baada ya mtu kuacha kuwa mteja.
Kuna nyakati tutaficha utambulisho wa data zako (ili zisiunganishwe na utambulisho wako) kwa ajili ya madhumuni ya utafiti au takwimu, na kwa kipindi hicho tunaweza kutumia data zako bila kukutaarifu kadiri tunavyohitaji kufanya hivyo.
8. Haki zako Kisheria
Zaidi ya haki zako chini ya sheria za ulinzi wa data na pale tunapotakiwa na kuwajibika kisheria, tutakupa, utakapoomba nakala ya data zako binafsi na tutarekebisha makosa yoyote utakayoyasema. Na kutokana na baadhi ya vifungu vya sheria, una haki ya kusema data zako binafsi ambazo zimekosewa zirekebishwe na kupinga au kuzuia matumizi yetu ya data zako binafsi.
Tunaweza kukutaka uthibitshe utambulisho waok kwa kutupati nakala ya kitambulisho halali ili kutimiza wajibu wetu wa kiulinzi na kuzuia kitendo cha kutoa data nje ya misingi ya sheria. Tuna haki ya kukutoza ada kwa maombi ya ziada kuhusu kupata data zako, na kwa kila nakala ya ziada ya data zako binafsi utakazoomba.
Maombi haya yote yakiwemo maombi ya kubadili data zako binafsi au maswali yoyote kuhusu sera hii na uwajibikaji wetu katika kumudu data zako, yanatakiwa kupelekwa: ghorofa ya 6, Block C, Plot no:198 Michenzani Mall, Mjini Magharibi, P.O Box 3850, Unguja, Zanzibar
9. Faharasa
MISINGI YA KISHERIA
Mapendeleo ya Haki humaanisha mapendeleo ya biashara yetu katika kutekeleza na kusimamia biashara yetu ili tuweze kukupa huduma na bidhaa bora zaidi. Tutahakikisha tunayatuliza madhara yoyote yanayoweza kukupata wewe (chanya na hasi) na haki zako kabla hatujachakata data zako binafsi kwa mapendeleo yetu binafsi. Hatutatumia data zako pale ambapo matumizi hayo yatakuhatarisha wewe (isipokuwa pale tu tunapopata ridhaa yako au tunapotakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria) Unaweza kupata taarifa za ziada juu ya namna tunavyochunguza mapendeleo yetu dhidi ya hatari na madhara yanayoweza kukupata tukitumia data zako kwa kuwasiliana nasi.
Utendaji wa Mkataba unamaanisha kuchakata data zako pale tu inapotusaidia kutendea kazi majukumu yetu ya kimkataba tulioingia nao pamoja na wewe au tunaotaka kuingia na wewe.
Kuzingatia Wajibu wa Kisheria inamaanisha kuchakata data zako binafsi pale inapotubudi kufanya hivyo kutimiza wajibu wetu wa kisheria.
WAHUSIKA WA TATU
Wahusika wa Tatu wa Ndani
Makampuni mengine ndani ya World Mobile Chain Ltd yakifanya kazi kama wasimamizi na wachakataji waliopo ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa huduma ya teknohama na utawala wa mifumo na kutoa ripoti za uongozi.
Wahusika wa Tatu wa Nje
- Watoa huduma wakifanya kazi kama wachakataji waliopo ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotoa huduma za teknohama na utawala wa mifumo mbalimbali.
- Washauri wakitaalamu wanaofanya kazi kama wachakataji wakiwemo wanasheria, watu wa benki, wakagua mahesabu na watoa bima waliopo ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotoa ushauri, huduma za kibenki, kisheria na mahesabu.
- Mamlaka za Kodi, wadhibiti wa serekali na mamlaka nyingine zinazofanya kazi kama wachakataji au watawala Pamoja nasi waliopo ndani ya Jamhuri ya Muunga wa Tanzania watakaohitaji kuripoti shughuli za uchakataji katika mazingira Fulani.