Vigezo na Masharti ya Huduma
Tafadhali soma vigezo na masharti ya huduma zetu, humu zinaitwa (“Vigezo” au “Huduma”) kwa umakini kabla ya kutumia programu ya World Mobile na huduma zinazotolewa na World Mobile Chain Limited, humu ikiitwa (“WM” “sisi” au “Ya Kwetu”)
Uwezo wako wa kupata huduma unategemea maamuzi yako kukubali na kuzingatia vigezo hivi. Vigezo hivi vinawahusu wageni wote, watumiaji, na wote wanaotumia huduma zetu. Kwa kutumia huduma zetu, unakubali kufungwa na vigezo hivi. Kama unapingana na kigezo chochote kile, basi hutoweza kutumia huduma zetu.
1. Usajili wa Mtumiaji
Unatakiwa kujisajili na huduma hii. Unakubali kuweka neno lako la siri liwe siri na utawajinika katika matumizi ya neno lako la siri na akaunti yako. Tuna haki ya kutoa, kurudisha, au kubadilisha jina la mtumiaji utakalochagua, kama tukiona jina hilo halifai, lina asili ya tusi, au ni jina linalopingika.
2. Data za Mtumiaji
Tutatunza data maalumu unazotuma Kwenye huduma zetu ili tuwe na uwezo wa kumudu huduma na data zinazohusiana na matumizi yako ya huduma zetu. Japokuwa tuna tabia ya kuweka hifadhi ya ziada ya data mara kwa mara, wewe ndio unayewajibika kimsingi kwa utunzaji wa data zako zote unazotuma kwenye matumizi ya huduma zetu. Unakubali kuwa, hatutawajibika kwako pale data hizi zitakapopotea au kuharibika.
3. Manunuzi
Malipo yote yanapelekwa kwa wahusika wa tatu wasiondeshewa na WM wanaotoa huduma za kuchakata malipo au tovuti za kuchakata malipo ya huduma au bidhaa zetu. Hatutunzi taarifa zozote za malipo, na hatuendeshi programu au tovuti hizi za malipo, hivyo hatuwajibiki kwa data zao au sera zao za faragha. Tunakusihi kuchambua sera yao ya faragha iliyowekwa Kwenye tovuti yao kabla hujatumia tovuti yao na kabla hujatoa taarifa zako binafsi au taarifa za mtu mwingine.
4. Kuvunja
Tunaweza kuvunja au kusitisha uwezo wako kupata huduma zetu, bila kutoa onyo kwa sababu yoyote ile, ikiwemo lakini bila vizingiti, ukavunja vigezo na masharti ya huduma zetu.
Vipengere vyote vya vigezo ambavyo kwa asili yake inabidi vidumu hata baada ya kuvunja makabaliano vitadumu, ikiwemo lakini bila vizingiti, vipengele vya umiliki, angalizo la waranti, fidia na mipaka ya uwajibikaji.
5. Maudhui
Huduma zetu zinaweza kukuruhusu kuchapisha, kujumuisha, kuhifadhi, kusambaza na kufanya baadhi ya taarifa zipatikane, ikiwemo, maandishi, picha, video, na maudhui mengineyo.
6. Shughuli Zisizoruhusiwa
Hutakiwi kutumia huduma kwa malengo yoyote yale zaidi ya yale ambayo tumeidhinisha ndio matumizi sahihi ya huduma zetu.
Kama. Mtumiaji wa huduma hii, unakubali kutokufanya yafuatayo:
- Kutafuta njia mbadala, kusimamisha, au kwa namna yoyote ile kuingilia mifumo yoyote ile ya ulinzi ya huduma hii, ikiwemo vipengere vinavyozuia uwezo wa kutumia au kunakili maudhui yoyote au kulazimisha udhibiti katika matumizi ya huduma na/au maudhui yaliyomo humo ndani.
- Kudanganya, kutapeli au kutupeleka pasipo sisi na watumiaji wengine, hasa katika jitihada ya kujifunza taarifa nyeti za akaunti za watumiaji kama vile neno/neno la siri.
- Kuwa na mtumizi yasiyo sahihi ya huduma zetu au kuripoti taarifa za uongo za utovu wa nidhamu au unyanyasaji.
- Kujihusisha na huduma zozote zinazofanywa na akili ya mfumo, kama vile kutumia hati kutuma maoni au ujumbe au kutumia vifaa kama vile uchimbaji wa data, roboti, au huduma za kukusanya data.
- Kuingilia, kuvuruga, au kutengeneza mzigo usiostahili katika mtandao au huduma mbalimbali zilizounganishwa na huduma yetu.
- Kujaribu kuiba utambulisho wa mtumiaji mwingine au kutumia jina la mtumiaji mwingine.
- Kuuza au kuhamisha wasifu wako
- Kutumia taarifa zozote zilizotolewa Kwenye huduma yetu kunyanyasa au kumdhuru mtu mwingine.
- Kutumia huduma hii kama sehemu ya jitihada ya kushindana na sisi au kutumia huduma na/au maudhui yake kutengeneza fedha au kibiashara.
- Rahisisha kuelewa, weka wazi chanzo, sambaratisha vipande, au tengeneza upya sehemu yoyote ya programu iliyo sehemu ya huduma hii.
- Kujaribu kuruka vizingiti vyovyote vilivyowekwa kuzuia uwezo wa kupata huduma, au sehemu yoyote ya huduma.
- Kunyanyasa, kuudhi, kubughudhi au kutisha wafanyakazi au mawakala wowote wanaohusika katika kutoa huduma.
- Kupakia au kusambaza (au kujaribu kupakia au kusambaza) virusi, farasi wa Trojan, au chochote kile, ikiwemo matumizi yaliyozidi ya herufi kubwa na barua takataka (kupakia maneno yanayojirudia) ambayo inaingilia matumizi ya watumiaji wengine na uwezo wao wa kuburudika na huduma, au iwe inaboresha, kudhoofisha, kuvuruga, kubadlisha au kuingilia matumizi, sifa, kazi, oparesheni au maboresho ya huduma.
- Pakia au sambaza (au kujaribu kupakia au kusambaza) kitu chochote kile kinachofanya kazi kama kikusanya taarifa kilicho hai au kilicholala, ikiwemo lakini bila vizingiti, vitu kama clear graphics interchange (“gifs”), pizeli 1×1, wadudu wa tovuti, vidakuzi au vifaa vinavyofanana navyo (wakati mwingine vinaitwa “vipelelezi pepe” au “passive collection mechanisms” or “pcms”)
- Isipokuwa inapokuwa ni matokeo ya matumizi ya viwango vya injini ya kutafuta, au matumizi ya kipekuzi cha mtandao, kutumia, kuzindua, kutengeneza, au kusambaza mfumo wowote ule, ikiwemo lakini bila kizingiti, buibui yoyote yule, matumizi ya kudanganya, mpapuro, au kisomaji kilicho nje ya mtandao kinachopata huduma, au kutumia au kuzindua hati iliyozuiliwa au programu nyingine.
- Kuharibu au kuchafua kwa namna yoyote ile, kwa maoni yetu, sisi au huduma yetu.
- Kutumia huduma nje ya namna yoyote ile inayopingana na yale yanayokubaliwa na sheria.
7. Haki za Hatimiliki
Isipokuwa imeidhinishwa vinginevyo, huduma tunayotoa ni mali yetu na kodi zake zote za asili, hifadhidata zake, uwezo wake wa kufanya kazi, tovuti yake muundo na michoro ya programu zake, sauti, video, maandishi, picha, na michoro yote katika huduma (kwa ujumla, “maudhui”) na alama zake za biashara, alama za huduma, na nembo zake zinamilikwa au kuendeshwa na sisi au tumepewa dhamana na leseni ya kuziendesha na hivyo tunalindwa na sheria za alama za biasha na sheria nyingine za hatimiliki na sheria za ushindania usio na uwiano za nchi ya Mauritius, nchi za kigeni na makongamano ya kimataifa. Maudhui na Alama zinatolewa katika huduma “KAMA ZILIVYO” kwa matumizi yako binafsi tu. Isipokuwa vinginevyo kama ilivyoorodheshwa Kwenye Vigezo vya Matumizi, hakuna sehemu ya Huduma au Maudhui au Alama inayoweza kunakiliwa, kuzalishwa upya, kuchapishwa upya, kupandishwa, kuchapishwa, kuonyeshwa wazi, kutafsiriwa, kusambazwa, kuuzwa, kuwapa wengine dhamana ya kutumia, au kwa namna yoyote iile kutumiwa kwa lengo la kutengeneza fedha bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mmliki.
Kama unakidhi matakwa ya kutumia huduma, unapewa leseni inayokuruhusu kupata huduma, kuitumia na kupakua au kuchapisha nakala ya sehemu yoyote ya maudhui ambayo umepata nafasi ya kuyatumia kwa matumizi yako binafsi, yasiyo na malengo ya kutengeneza fedha. Tunahifadhi haki zetu zote ambazo hujapewa wewe kuhusiana na Huduma, Maudhui na Alama.
8. Viungo Kwenda Tovuti Nyingine
Huduma zetu zinaweza kuwa na viungo vinavyokupelekea Kwenye tovuti za wahusika wa tatu, ambazo hazimilikiwi wala kuendeshwa na sisi.
Hatuna udhibiti, na hutuchukui jukumu lolote lile kuhusu maudhui, sera za faragha, au utendaji wa tovuti yoyote ile ya wahusika wa tatu au huduma zao. Unakubali na kukiri kuwa WM haitawajibika, moja kwa moja na vinginevyo, kwa uharibifu au hasara yoyote ile itakayotokana au itakayosemekana imetokana na au imekuwa matokeo ya matumizi au uhusihswaji na maudhui, huduma na bidhaa zinazopatikana katika tovuti hizo na huduma zake.
9. Maboresho na Usumbufu
Tuna haki ya kubadilisha au kuondoa maudhui ya Huduma, muda wowote ule au kwa sababu yoyote ile kwa maamuzi yetu wenyewe bila onyo. Walakini, hatuna wajibu wowote ule wa kususiha taarifa zozote zile za Humuda yetu. Pia, tunahifadhi haki ya kuboresha au kusitisha Huduma yote au sehemu ya huduma pia onyo wakati wowote ule. Hatutawajibika kwako au kwa mhusika yoyote yule wa tatu kwa maboresho yoyote, mabdiliko ya bei, au kusitishwa kwa huduma.
Hatuwezi kutoa uhakika kuwa Huduma itapatikana muda na wakati wote. Tunaweza kupata changamoto za vifaa au programu na tukahitajika kufanya maboresho/matengenezo yanayohusiana na Huduma, nah ii kupelekea kusitisha kwa huduma, au uchelewaji wa kasi ya huduma. Tunahifadhi haki ya kubadilisha, kurekebisha, kusasiha, kusitisha, kusimamisha, na kwa namna yoyote ile kuboresha Huduma muda wowote na kwa sababu yoyote ile bila kutoa onyo kwako. Unakubali kuwa hatuwajibiki kwa namna yoyote ile kwa hasara, uharibifu au ghasia yoyote ile inayosababishwa na wewe kutoshindwa kupata Huduma kipindi hiki cha Huduma kutopatikana. Hakuna kitu katika Vigezo Hivi vya Matumizi kutamaanisha kuwa sisi tunawajibika kutoa huduma, usasiha unaohusiana na haya yote.
10. Marekebisho
Kunaweza kuwa na taarifa katika Huduma ambazo zinajumuisha makosa, kukosekana pamoja na vitu visiyo sahihi vinavyohusiana na Huduma, ikiwemo, maelezo, bei, upatikanaji, na taarifa nyingine za ziada. Tuna haki ya kurekebisha makosa yoyote yale, au taarifa zilizokosekana na kubadilisha au kusasiha taarifa Kwenye Huduma muda wowote ule, bila kutoa onyo.
12. Fidia
Unakubali kutetea, kufidia, na kutoona hatia yoyote kwetu, mashirika yetu, wanaohusika nasi, na maafisa wetu, mawakala wetu, washirika wetu na wafanya kazi wetu, kutokana na hasara yoyote ile, uharibifu na madai ikiwemo ada ya wanasheria na matumizi yaliyofanywa na wahusika wa tatu zinazotokana na sababu zifuatazo:(1) Matumizi ya Huduma; (2) Kuvunja Vigezo hivi vya Matumizi; (3) kuvunja uwakilishi na waranti zozote zile zilizojumuishwa katika Vigezo hivi vya Matumizi(4) Uvunjwaji wako wa haki za wahusika wa tatu, ikiwemo lakini bila vizingiti kwa hatimiliki(5) Kitendo chochote kile cha kudhuru kwa mtumiaji mwingine yoyote wa Huduma uliyeunganishwa naye kupitia Huduma yetu. Tunahifadhi haki, kwa gharama zako, kusimamia utetezi na udhibiti wa jambo lolote lile ambalo wewe unatakiwa utupe fidia, na unakubali kuonyesha ushirikiano, kwa gharama zako, na utetezi wetu wa shutuma hizo. Tutatumia jitihada madhubuti kukujulisha kuhusu shutuma hizi pale tutakapozitambua.
13. Mengineyo
Hivi vigezo vya matumizi au sheria zozote za uendeshaji zilizochapishwa na sisi kuhusu Huduma zinajumuisha makubaliano yote na makubaliano kati yetu na wewe. Pale tutakaposhindwa kutenda na. kusimamia haki yoyote ile katika Hivi Vigezo vya Matumizi haitamaanisha kuwa haki hizo hazipo tena. Vigezo hivi vinafanya kazi sambamba na sheria. Tunaweza hamisha haki zetu zote au sehemu ya haki zetu kwa wengine muda wowote. Hatutawajibishwa kwa hasara, uharibifu, ucheleweshwaji uliosababishwa na jambo lolote lile lililo nje ya uwezo wetu wa kudhibiti. Kama sehemu yoyote ile ya Vigezo hivi vya Matumizi inaonekana kuwa sio sahihi kisheria, kipengere hicho cha Vigezo kitatolewa katika makubaliano haya na hakitaathiri vipengere vingine vya Makubaliano haya. Hakuna mahusiano ya kibiashara, uwakili, ajira wala uwakala yanayotengezwa kati yetu na wewe kama matokeo ya Vigezo hivi vya Matumizi au utumiaji wa Huduma zetu. Unakubali kuwa Vigezo hivi vya Matumizi havitatumika dhidi yetu kwasababu sisi tumeviandika. Kwahiyo unaachia haki ya utetezi wowote ule unaoweza kuwa nao kwa misingi ya Vigezo hivi vya Matumizi na kitendo cha kutoweka sahihi katika Makubaliano haya.
14. Wasiliana nasi
Kutatua malalamiko kuhusu huduma zetu au kupokea taarifa za ziada kuhusu matumizi ya huduma, tafadhali wasialiana nasi kupitia:
World Mobile Chain Ltd
Ghorofa ya 6, Block C, Michenzani Mall
Karume Road
Mjini Magharibi
Unguja, Zanzibar
P.O Box 3850
TIN no. 149-548-777
ZRB no. Z025785573
VRN no. 07003545W
Simu: 0800 110220
Barua pepe: [email protected]